IQNA

Sayyed Hassan Nasrallah:

Marekani inazuia kuangamizwa kikamilifu kundi la kigaidi la ISIS

11:19 - October 10, 2017
Habari ID: 3471211
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Marekani inazuia kuangamizwa kikamilifu kundi la kigaidi la Daesh au ISIS huko Syria na inalisaidia kundi hilo kwa silaha kupitia kituo vituo vyake vya kijeshi vilivyo Syria kinyume cha sheria.

Sayyid Hassan Nasrullah aliyasema hayo Jumapili jioni katika shughuli ya kuwakumbuka makamanda wawili wa Hizbullahwaliouawa shahidi wiki iliyopita wakipambana na kundi la ISIS. Amesema kuwa kwa sasa wapiganaji wa kundi la Daesh wako katika sehemu moja ya mji wa Deir al Zour huko Syria na kwamba Marekani inataka kurefesha umri wa kundi hilo.

Sayyid Nasrullah amesema kuwa Marekani haitaki kuona kundi hilo likiangamizwa kikamilifu na kwamba, jeshi la nchi hiyo linazuia wanajeshi wa Syria na wapiganaji wa Hizbullah kusonga mbele kwenye maeneo yanayodhibitiwa na Daesh huko Syria.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza udharura wa kuangamizwa kabisa kundi la kiwahabi na kitakfiri la ISIS na kusema: Kama saratani hiyo haitaangamizwa kikamilifu itarejea tena katika maeneo iliyokuwa ikiyadhibiti na kufanya mauaji ya kigaidi. Hata hivyo amesisitiza kuwa, njama hizo za Marekani hazitafua dafu na kwamba uhai wa kundi la Daesh unakaribia mwisho.

Kuhusu uhasama wa siku nyingi za Washington dhidi ya Tehran, Sayyid Nasrullah amesema:Tatizo la Marekani na Iran halihusiani na kadhia ya nyuklia bali tatizo ni changamoto kubwa inayotolewa naIran dhidi ya miradi na mipango ya Marekani na Saudi Arabia katika eneo la Asia Magharibi.

3650555

captcha