IQNA

Mufti wa Libya alaani namna Saudia inavyowadhulumu wanazuoni wa Kiislamu

19:33 - February 07, 2018
Habari ID: 3471383
TEHRAN (IQNA)-Mufti mkuu wa Libya amelaani vikali namna utawala wa kifalme Saudia unavyowakandamiza wanazuoni wa Kiislamu.

Katika ukosoaji nadra,  Mufti wa Libya Sheikh Sadiq al-Ghairani ameandika makala na kuwataja watawala wa Saudia na waungaji mkono wao kuwa madhalimu na matwaghuti.

Amesema utawala wa kifalme Saudia unawakamata na kuwafunga jela Maulamaa wa Kiislamu na hata inawapelaka katika jela za nchi zingine.

Raia kadhaa wa Libya ni kati ya wanazuoni wa kimapinduzi wa Libya wamekamatwa Saudia Arabia katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani  (Juni 2017) na hadi sasa hawajulikani waliko.

Hivi karibuni Jumuiya ya Kimataifa ya Wanazuoni Waislamu (IUMS) ililaani tawala za Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kuendelea kuwashikilia kinyume cha sheria wahubiri wa Uislamu.

Katika taarifa IUMS imelaani vikali kushiliwa pasina kufunguliwa mashtaka wanazuoni hao na imetaka waachiliwe huru mara moja kwani hakuna kosa walilofanya sipikuwa tu walibainisha wazi mitazamo yao.

Taarifa hiyo imetolwa baada ya kuenea habari kuwa ya kulazwa hospitalini Salman al-Ouda, mmoja wa shakhsia wakubwa wa upinzani na kidini nchini Saudi Arabia ambaye miezi minne iliyopita, alitiwa mbaroni kwa amri ya Mohammed bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo.

3689413

captcha