IQNA

Serikali ya Senegal yafadhili vituo vipya vya Qur'ani

10:09 - February 09, 2018
Habari ID: 3471385
TEHRAN- (IQNA) Serikali ya Senegal imetangaza mpango wa kuanzisha vituo vipya 21 vya Qur'ani tukufu katika mji wa Kaffrine, kati mwa nchi hiyo.

TEHRAN (IQNA)-Serikali ya Senegal imetangaza mpango wa kuanzisha vituo vipya 21 vya Qur'ani tukufu katika mji wa Kaffrine, kati mwa nchi hiyo.

Taarifa zinasema Rais wa Senegal ameidhinisha  bajeti ya kujengwa vituo hivyo vya kufundisha Qur'ani katika mji huo ambao pia ni maarufu kwa lakabu ya 'Mji wa Elimu'.

Kwa mujibu wa Bw. Mbaba Ma, mwenyekiti wa wa akademi ya sayansi katika mji huo, kuanzishwa vituo hivyo vipya vya Qur'ani kutapelekea kuimarika masomo ya Qur'ani na Kiislamu katika mji huo na Senegal kwa ujumla.

Mbali na kutoa mafundisho ya Qur'ani na Kiislamu, vituo hivyo  pia vitatoa mafunzo mengine. Mji wa Kaffrine ni mji mkuu wa eneo la Kaffrine kati mwa Senegal na ni eneo ambalo pia ni mashuhuri kwa ukulima.

Senegal ni nchi iliyo katika eneo la Afrika magharibi na inapakana na Mauritania uapnde wa Kaskazini, Mali upande wa Mmashariki, Guinea upande wa kusini mashariki na Guinea-Bissau Upande wa kusini Magharibi katika hali ambayo nchi ya Gambia ni kanda kati kati mwa Senegal ikiunganishwa na mipaka ya kimatiafa kupitia Bahari ya Atlantiki.

3689462

captcha