IQNA

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran katika Mwezi wa Ramadhani

20:04 - May 14, 2018
Habari ID: 3471513
TEHRAN (IQNA) – Maonyesho ya 36 ya Kimataifa ya Qur'ani ambayo hufanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani yamepangwa kuanza Mei 19.

Akizungumza na waandishi habari siku ya Jumatatu, mkuu wa maonyesho hayo, Abdul-Hadi Faqihizadeh amesema taasisi 20 za kimataifa za Qur'ani zimealikwa katika maonyesho ya mwaka huu.

Ameongeza kuwa wanazuoni na wataalamu 26 maarufu wa Qur'ani Tukufu kutoka nchi saba, zikiwemo Iraq, Russia, Uturuki na Malaysia wanatazamiwa kushiriki katika maonyesho yam waka huu.

Maonyesho ya 26 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran yamepangwa kuanza Mei 19 hadi Juni 4 katika Ukumbi wa Sala (Musalla) wa Imam Khomeini MA mjini Tehran.

Faqihizadeh amesema maonyesho hayo ni makubwa zaidi ya aina yake duniani na mada yake kuu ni Qur'ani Tukufu.

Amesema wizara 14, taasisi 32 za Qur'ani Tukufu, vyuo vikuu 16 na vyuo 15 vya kidini (Hawza) vinashiriki katika kuandaa maonyesho hayo.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran hufanyika kila mwaka katika siku za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa lengo la kuimarisha  fikra za Qur'ani Tukufu na harakati zinazohusiana na Qur'ani Tukufu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

3714229

captcha