IQNA

Nakala milioni moja za Qur'ani zasambazwa katika Msikiti wa Makka msimu wa Hija

23:30 - August 17, 2018
Habari ID: 3471632
TEHRAN (IQNA)- Nakala milioni moja za Qur'ani Tukufu zimesambazwa miongoni mwa Waislamu waliofika katika Msikiti wa Makka maarufu kama Masjid al-Haram katika msimu wa Hija mwaka huu.

Taarifa zinasema nakala hizo za Qur'ani Tukufu zimesambazwa na idara inayosimamia Msikiti wa Makka na ni katika sehemu ya huduma zinazotolewa kwa waumini waliofika katika Nyumba Tukufu ya Allah SWT kutekeleza Ibada ya Hija.
Idara ya ya Masuala ya Misahafu na Vitabu Katika Masjid al-Haram imesema nakala hizo za Qur'ani pia zina tarjama za lugha mbali mbali na pia kuna nakala za Qur'ani za Braille maalumu kwa watu wenye ulemavu wa macho.
Idara hiyo imetnagaza pia kuwa itajitahidi kutoa huduma bora zaidi kwa mahujaji wa Nyumba ya Allah na kwamba jitihada zote zinafanyika kufanikisha jambo hilo.
Waislamu takribani milioni mbili kutoka maeneo yote ya dunia wameshawasilia Saudi Arabia kwa ajili ya Ibada ya kila mwaka ya Hija.

3739007

captcha