IQNA

Kofi Annan, Katibu Mkuu wa zamani wa UN aaga dunia

15:45 - August 18, 2018
Habari ID: 3471634
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amefariki dunia nchini Uswisi baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Annan ambaye  ameaga dunia akiwa na miaka 80 alikuwa ni Mwafrika mweusi wa kwanza kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, akihudumu mihula miwili kuanzia mwaka 1997 hadi 2006.

Baadaye akahudumu kama mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria na kuchangia kupatikana kwa suluhu la amani la mzozo wa nchi hiyo. Annan aliwahi kupewa tuzo ya kimataifa ya Amani ya Nobel mnamo mwaka 2001

Taarifa kutoka kwa familia na kwenye wakfu wa Kofi Annan ilitangaza kifo chake siku ya Jumamosi asubuhi. Katika taarifa kupitia kwenye mtandao wa kijamii, taarifa hiyo ilisema "Kofi Annan, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na aliyewahim kupewa tuzo ya Amani ya Nobel ameaga dunia leo Jumamosi" baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Familia inaomba faragha wakati huu wa maombolezo na mipango ya kuenzi maisha yake pamoja na mipango ya msiba itatangazwa baadaye. Mke wake bi Nane na watoto wao Ama, Kojo na Nina walikuwa pamoja naye wakati umauti ulipomfika. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema amesikitishwa sana na habari za kifo cha mtangulizi wake akimtaja kuwa alikuwa ni "nguvu iliyoongoza kwa mema".

Kofi Atta Annan na dada yake Efua Atta, walizaliwa kwenye mji wa Kumasi katika nchi ambayo wakati huo ilikuwa inajulikana kama Gold Coast Aprili mwaka 1938. Majina ya pacha hao yaliamaanisha kuwa walizaliwa Ijumaa huku majina yao ya kati yakimaamisha kuwa waliukuwa ni pacha.

3739438

captcha