IQNA

Iran: Walipa kodi Marekani wanafadhili kundi la kigaidi la MKO

8:35 - June 29, 2020
Habari ID: 3472909
TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema nchi za Ulaya na Marekani ni washirika wa kundi la kigaidi la Munafikin (MKO) katika mauaji ya watu wa Iran.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilitoa taarifa kupitia ukurasa wa Twitter siku ya Jumapili kwa mnasaba wa "Wiki ya Haki za Binadamu za Kimarekani"  na kusema Kundi la Munafikin (MKO) ni kundi la kigaidi na utumiaji mabavu. Taarifa hiyo imeongeza kuwa nchi za Ulaya zimelipatia hifadhi na himaya kundi hilo la waasi ambapo fedha za walipa kodi wa Marekani ndizo zinakidhi mahitaji ya kundi hilo katili.

Itakumbukwa kuwa katika muongo wa 80, mashambulizi ya kuogofya ya kigaidi  yalijiri nchini Iran kwa himaya ya Marekani baina ya Juni 26 na Julai 3 ambapo kipindi hicho katika kalenda ya Iran kimepewa jinai la 'Wiki ya Haki za Binadamu za Kimarekani". Katika kipindi hiki huwa kunafichuliwa jinai za Marekani na hadaa za nchi hiyo kuhusu haki za binadamu. 

IkumbukwE kuwa  28 Juni 1981 kulijiri hujuma ya kigaidi katika ofisi ya Chama cha Jamhuri ya Kiislamu mjini Tehran ambapo maafisa  73 wa ngazi za juu wa serikali waliuawa kigaidi katika hujuma ya kundi la kundi la kigaidi la MKO. Aidha  28 Juni 1987, utawala wa Iraq wa kibaath uliokuwa ukiongozwa na Saddam ulitekeleza hujuma ya silaha za kemikali dhidi ya Iran na kuua idadi kubwa ya raia. Saddam alikuwa akipata uungaji mkono wa nchi za Magharibi na silaha za kemikali alizotumia alizinunua kutoka nchi hizo za Magharibi zikiongozwa na Marekani. Katika jinai nyingine, mnamo Julai 3 1988, ndege ya abiria ya Iran ililengwa kwa kombora kutoka manowari ya Jeshi la Majini la Marekani katika Ghuba ya Uajemi ambapo raia wote 290 waliokuwa ndani ya ndege hiyo, wakiwemo wanawake na watoto walipoteza maisha. Hiyo ni baadhi tu ya mifano ya hatua zilizo dhidi ya ubinadamu za Marekani dhidi ya watu wa Iran.Iran: Walipa kodi Marekani wanafadhili kundi la kigaidi la MKO

3907473

captcha