IQNA

Waislamu watakiwa kudumisha umoja katika Mwezi wa Ramadhani + Video

15:01 - April 25, 2021
Habari ID: 3473847
TEHRAN (IQNA)- Mwanazuoni wa ngazi za juu wa Kiislamu ametoa wito wa kudumishwa umoja wa umma wa Waislamu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kukabiliana na njama za maadui.

Sheikh Dkt. Ali Mohyiddeen Al-Qaradaghi katibu mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wanazuoni wa Kiislamu amezungumza kwa njia ya video na IQNA na kusema Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni fursa nzuri ya kutekeleza maamurisho ya Mwenyezi Mungu SWT kuhusu kustawisha umoja na mshikamano wa Waislamu.

Ameashiria sehemu ya Aya ya 103 ya Sura Aal Imran katika Qur’ani Tukufu isemayo,  “Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane…”Amesema aya hii ni amri ya wazi ya Mwenyezi Mungu SWT kuhusu ulazima wa kuwepo umoja na mashikamano wa Kiislamu.

Aidha ameashiria sehemu ya aya ya pili ya Surah al Maida isemayo:”…  Na saidianeni katika wema na uchamngu…” na kuongeza kuwa aya hii inawahimiza Waislamu kushirikiana na kusaidiana.

Sheikh Qaradaghi amesema ushirikiano na umoja ni nguzo muhimu za Waislamu katika kukabiliana na changamoto na maadui. Ameongeza kuwa njia muhimu ya kuweza kuleta umoja huo ni kuzingatia misingi ya  Taqwa, Ikhlasi na Tawhidi.

3965631

Kishikizo: waislamu umoja Qaradaghi
captcha