IQNA

Ongezeko la asilimia 9 la chuki dhidi ya Uislamu Marekani

21:33 - April 27, 2021
Habari ID: 3473855
TEHRAN (IQNA)- Nchini Marekani kumeshuhudiwa ongezeko la asilimia 9 ya idadi ya malalamiko ya unyanyasaji dhidi ya Waislamu ambayo yalipokewa mwaka uliopita wa 2020 ikilinganishwa na mwaka wa kabla yake.

Hayo yamedokezwa na  Baraza la Uhusiano wa Amerika na Uisilamu (CAIR) ambalo linaloongoza kwa kutetezi haki za Waislamu nchini Marekani.

Taarifa iliyotangazwa na CAIR Jumatatu  imesema kuwa ilipokea malalamiko 6,144 kitaifa mnamo 2020, ambayo ilisema yanahusu maswala mbalimbali ikiwa ni pamoja na "ubaguzi, vizuizi vya uhamiaji na kusafiri, visa vya upendeleo, masuala yanayohusiana na haki za wafungwa, utekelezaji wa sheria na kadhalika.

Taarifa ya CAIR imesema kuwa, malalamiko 1,814 yanahusiana na unyanyasaji unaohusiana na masuala ya uhamiaji  na safari, ambayo yalichukua sehemu kubwa zaidi ya malalamiko yaliyowasilishwa na Waislamu wa Marekani. Malalamiko mengine 1,151 yalihusiana na ubaguzi, na nusu nyingine ya idadi hiyo ilihusu suala la kubaguliwa Waislamu katika masuala ya ajira.

Siku chache zilizopita jumuiya na makundi ya Kiislamu ya Marekani yaliitaka serikali ya nchi hiyo kuteua mwakilishi maalumu wa kusimamia na kukabiliana na chuki na propaganda chafu dhidi ya dini ya Uislamu nchini humo.

Ripoti ya USA Today inasema kuwa, Baraza la Jumuiya za Kiislamu nchini Marekani limemwandikia barua Rais wa nchi hiyo, Joe Biden likisisitiza kuwa, kuwepo mwakilishi maalumu wa kusimamia na kupambana na chuki na propaganda chafu dhidi ya Uislamu katika Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje kunaweza kusaidia juhudi za kupata suluhisho la tatizo hilo ambalo linaizonga jamii ya Waislamu nchini Marekani. 

Ikulu ya Rais wa Marekani, White House hadi sasa haijatoa jibu iwapo serikali ya nchi hiyo itateuwa mwakilishi maalumu wa kushughulikia chuki na propaganda chafu dhidi ya Uislamu au la. 

Wiki iliyopita Rais Joe Biden alikiri katika ujumbe wake uliotolewa kwa mnasaba wa kuwadia mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwamba, Waislamu wanaudhiwa na kubughudhiwa katika jamii ya Marekani.

3967495

Habari zinazohusiana
captcha