IQNA

Wachezaji wa Ligi ya Premier waruhusiwa kufungua saumu katikati ya mechi + Video

19:19 - April 30, 2021
Habari ID: 3473862
TEHRAN–(IQNA) -  Ligi Kuu ya Soko Uingereza(England)-EPL-, imewaruhusu wachezaji Waislamu kufungua suamu ya Mwezi Mtukufu waRamadhani kati kati ya mechi.

Tukio hilo limejiri kwa mara ya kwanza Jumatatu 26 Aprili wakati wa mechi baina ya Licester City na Crystal Palace. Mechi hiyo ilikuwa ikiendelea wakati wa Magharibi na hivyo wachezaji Waislamu, Wesley Fofana na Cheikhou Kouyate waliruhusiwa kufungua saumu katikati ya mechi.

Kable ya mechi kuanza, timu hizo mbili zilikubaliana na refa wa mechi hiyo, Graham Scott kuwa mechi hiyo ingesimamiwsha baada ya nusu saa ili kuwaruhusu wachezaji hao wawili kufungua saumu yao ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Inaaminika kuwa hii ndio mara ya kwanza kabisa katika historia ya Ligi ya Premier ya Uingereza kwa mechi kusimamishwa ili kuwaruhusu wachezaji wa Uislamu kufunga saumu kwa kula na kunywa baada ya adhana ya wakati wa Magharibi.

Fofana ametuma ujumbe kwa njia ya Twitter na kutoa shukrani zake kwa waliofanikisha jambo hilo.

3967434

captcha