IQNA

Radio ya Qur'ani Sharjah yaandaa mashindano ya Qur'ani Mwezi wa Ramadhani

21:34 - May 04, 2021
Habari ID: 3473876
TEHRAN (IQNA)- Radio ya Qur'ani mjini Sharjah katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imeandaa mashindano ya Qur'ani Tukufu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa taarifa, washiriki katika mashindano hayo wanaiga sauti za qiraa ya Qur'ani Tukufu ya wasomi mashuhuri duniani.

Njia ya kushiriki ni kujirekodi na kisha kutuma klipi ili ushiriki katika mashindano. Baada ya klipu kusikilizwa na jopo la majaji wa Radio ya Qur'ani Sharjah washidi watatangazwa.

Lengo kuu la kuandaa mashindano kama hayo limetajwa kuwa ni kutambua wasomaji wenye vipaji na pia kutunza mbinu za qiraa za wasomaji maarufu duniani.

Washindano watapata zawadi ya UAE Dirhamu 50,000.

3474616

captcha