IQNA

Soko la Pamoja la Nchi za Kiislamu linawezaleta mabadiliko duniani

19:12 - October 25, 2021
Habari ID: 3474472
TEHRAN (IQNA)- Msomi wa Kiislamu kutoka Ubelgiji anasema kuna haja ya kuanzisha soko la pamoja la nchi za Kiislamu ili kuleta mabadiliko katika dunia.

Katika mahojiano na IQNA, Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyied Ziauddin Salehi Khansari, ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Maulamaa wa Kishia Ubelgiji amesema: "Tunahitaji uchumi wa pamoja wa Kiislamu kwa ajili ya umoja wa mataifa ya Waislamu."

Amesema kuundwa jumuiya ya kimataifa kwa lengo hilo kutaleta mabadliko makubwa kutokana na utajiri mkubwa katika nchi za Waislamu.

Akifafanua kuhusu maana ya umoja amesema kuhusu umoja wa kijamii, moja kati ya mafundisho ya Kiislamu ni kuhusu  umma ulioungana na kwamba neno umma limetumika sana katika Qur'ani.

Aidha amekumbusha kuhusu aya 103 ya Aal Imran katika Qur'ani kuhusu umoja inayosema: " Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka."

Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyied Ziauddin Salehi Khansari amesema matatizo mengi leo miongoni mwa Waislamu yamesbabaishwa na ukosefu wa umoja.

Ameongeza kuwa, moja kati ya changamoto katika ulimwengu wa Kiislamu ni mkakati wa baadhi ya madola ya Kiarabu kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unakalia ardhi za Palestina kwa mabavu. Amesema madola kama hayo hajiamini kwani yanahisi usalama wao utadhaminiwa kwa kuungana na utawala wa Kizayuni katika hali ambayo hakuna msingi katika dhana kama hiyo.

Amesema mabeberu hawataki kuona umoja baina ya Waislamu na hivyo wanaeneza hofu baina ya Waislamu ili waogopane na ameongeza kuwa, hiyo ni sera ambayo imekuwa ikifuatwa na mkoloni Muingereza kwa muda mrefu.

4005853

captcha