IQNA

Qiraa ya Qur'ani Tukufu ya Qarii wa Misri aliyeshiriki mashindano ya Tanzania

15:50 - May 02, 2022
Habari ID: 3475199
TEHRAN (IQNA)- Mohamed Ibrahim Ahmed Ghanim ni kijana Mmisri aliyeibuka mshindi katika shindano la qiraa katika Mashindano ya 22 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tanzania mwaka huu.

Mohammad aliibuka mshindi katika kategoria ya qiraa ya mashindano hayo na alipohojiwa alibainisha furaha yake kutokana na mafanikio hayo huku akimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumuwezesha kufikia moja kati ya malengo yake.

Ahmed Ghanim mbali na kuwa ni qarii mzuri wa Qur'ani Tukufu, halikadhalika pia amekihifadhi kikamilifu Kitabu hicho Kitukufu.

Ahmed Ghanim alizaliwa katika jimbo la Kafr el-Sheikh nchini Misri na alianza kujifunza Qur'ani Tukufu utotoni na alipofika miaka 14 alikuwa amehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Tokea utotoni alikuwa akisikiliza qiraa ya mabingwa wa Qur'ani kama vile  Sheikh Mohammad Raf’at na Sheikh Mustafa Ismail na anataka kuwa mrithi bora wa wanazuoni hao. Hivi sasa anaendeleza masomo yake ya Qur'ani Tukufu katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al Azhar.

4052622

captcha