IQNA

Katika mazungumzo na Rais wa Uturuki

Rais wa Iran asisitiza kuhusu jitihada za kimataifa kusitisha hujuma Israel dhidi ya Wapalestina

15:48 - May 03, 2022
Habari ID: 3475202
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyataja matukio ya karibuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina kuwa yasiyokubalika na kueleza kuwa: Kuna ulazima wa kufanyika juhudi za kusitisha mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina kupitia msaada wa nchi za Kiislamu na jitihada za kimataifa.

Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana Jumatatu alizungumza kwa simu na Rais Recep Tayyep Erdogan wa Uturuki na kutoa mkono wa heri na fanaka kwa taifa na nchi rafiki na jirani ya Uturuki kwa kuwadia Sikukuu ya Idul-Fitr na kueleza kuwa: Siasa za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kukuza uhusiano wa pande zote na nchi za kanda hii hususan Uturuki. 

Kwa upande wake Rais wa Uturuki Recep Tayyep Erdogan ametoa mkono wa baraka heri ya Idul-Fitr kwa taifa na serikali ya Iran na akasema kwamba, anataraji kuwa sikukuu hii  italeta afya, ustawi na furaha kwa Uimwengu wote wa Kiislamu. 

Rais wa Uturuki aidha ameeleza hamu yake ya kufanya ziara hapa Tehran na kuongeza kuwa: Uturuki inataka kufanya mazungumzo na kubadilishana mawazo na Iran kuhusu matukio ya kieneo na kimataifa na pia kutekeleza mipango ya kupanua ushirikiano wa pande mbili na kimataifa hasa kuzidisha kiwango cha biashara kati yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

4054554/

captcha