IQNA

Wasomaji Maarufu wa Qur'ani Tukufu /4

Qiraa ya Qur’ani ya Ustadh Minshawi ni bora na ya kipekee

23:08 - September 21, 2022
Habari ID: 3475818
TEHRAN (IQNA)- Qarii maarufu wa Qur’ani kutoka Misri,marhum Ustadh Sidiq Minshawi alikuwa na qiraa ambayo imedumu na inaendelea kuwavutia mamilioni hadi leo.

Mohammad Siddiq El-Minshawi ni maarufu kwa sauti yake yenye mvuto wa aina yake  na qiraa yake hutulia katika nyoyo za wasikilizaji.

El-Minshawi alizaliwa Januari 1920 katika mji wa Al Minshah katika jimbo la Sohag nchini Misri na alilelewa na kuinukia katika familia ya wasomaji Qur'ani. Alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 8 na mwaka mmoja baadaya akaanza kujifunza kusoma Qur'ani kitaalamu.

Baada ya muda usio mrefu Minshawi alipata umashuhuri kama qarii ambaye alikuwa akitumia mbinu za Tarteel na Tahqiq katika usomaji wake. Alisafiri katika nchi nyingi duniani kwa ajili ya usomaji Qur'ani zikiwemo Indonesia, Jordan, Saudi Arabia, Syria, Iraq, Pakistan na Sudan. Aliaga dunia mwaka 1969 akiwa na umri wa miaka 49.

Misri ni mashuhuri duniani kama nchi ambayo imeweza kutoa wasomaji bora zaidi wa Qur'ani Tukufu katika miongoi ya hivi karibuni.

3480569

captcha