IQNA

Zaidi ya Misikiti 100 yahujumiwa Uingereza

18:59 - November 22, 2016
Habari ID: 3470690
IQNA-Zaidi ya zaidi ya vituo vya Kiislamu na misikiti 100 imehujumiwa nchini Uingereza katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Kwa mujibu wa riopoti ya hivi karibuni ya taasisi moja ya kijamii ijulikanayo kama Tell MAMA, ambayo hufuatilia vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu Uingereza, kuanzia Mei 2013 hadi Septemba mwaka huu, kumekuwepo na hujuma zaidi ya 100 dhidi ya misikiti na vituo vya Kiislamu.

Ripoti hiyo imesema aghalabu ya hivuma hizo zinajumuisha uteketezaji moto wa makusudi, kumwaga nyama za nuguriwe katika maeneo hayo ya Kiislamu na vitendo vingine vingi vya utumiaji mabavu na vyenye kuwaudhi Waislamu. Kati ya vitendo hivyo ni kuandika maandishi yenye chuki dhidi ya Uislamu katika kuta za misikiti. Hujuma hizo hutekelezwa katika maeneo yenye Waislamu wengi na misikiti kote Uingereza. Aidha imebainika kuwa aghalabu ya hujuma hizo hutekelezwa na na makundi yenye misimamo mikali ya mrengo ya kulia.

Mwanzilishi wa Tell MAMA Fiyaz Mughal amesema chuki dhidi ya Waislamu inaelekezwa kwa misikiti ambayo ni nembo ya jamii za Waislamu Uingereza. Aidha amesema misimamo ya kufurutu ada ya makundi ya mrengo wa kulia ni chanzo kikuu cha hujuma hizo.

Mkureugenzi katika Tell MAMA, Iman Abou Atta ametoa wito kwa wasimamizi wa misikiti kuwa macho na kupasha habari kwa taasisi hiyo na idara za polisi iwapo watashuhudia hujuma.

Taasisi ya Tell MAMA ni mradi wa kitaifa wa Uingereza wenye lengo la kuripoti vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.

3548099

captcha