Yaslam al Maqari ambaye ni Mshauri wa Wizara ya Masuala ya Kiislamu nchini Mauritania ameandika katika ukurasa wake wa Twitter na Facebook kwamba: Wizara hiyo imewataka wasimamizi wa misikiti yote nchini kurusha hewani qiraa na visomo vya Qur'ani tukufu kupitia vipaza sauti vya misikiti.
Baada ya watu kadhaa kupatwa na virusi vya corona nchini Mauritania, serikali ya nchi hiyo imechukua hatua kadhaa za kukabiliana na janga hilo ikiwa ni pamoja na kufunga shule, kupiga marufuku safari za anga na kufunga baadhi ya mipaka ya nchi hiyo.
Idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa COVID-19 au corona kote barani Afrika imepindukia watu 1,114 katika nchi 40 barani humo.
Hadi kufikia Jumamosi iliyopita nchi za Misri, Afrika kusini na Algeria zilikuwa zikiongza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya virusi vya corona.