IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu Brunei kufanyika Machi

20:17 - February 14, 2023
Habari ID: 3476563
TEHRAN (IQNA) – Usajili umefunguliwa kwa ajili ya mashindano ya kitaifa ya Qur’ani Tukufu kwa vijana nchini Brunei, ambayo yataanza mwezi Machi.

Wizara ya Utamaduni, Vijana na Michezo ya nchi hii ya Kusini Mashariki mwa Asia kupitia Idara ya Vijana na Michezo itaandaa duru ya kwanza ya mashindano hayo Mei 10-13.

Washiriki wanaweza kuwa ni raia na wakaazi wa kudumu walio na umri wa kati ya miaka 15-30.

Washiriki wa mwaka huu hawapaswi kuwa miongoni mwa washindi wa mashindano yoyote ya kimataifa ya usomaji wa Qur'ani Tukufu ambayo huandaliwa na serikali ya Malaysia au Mashindano ya Kusoma Qur'ani Tukufu ya Asia ya Kusini Mashariki kwa Vijana ambayo huandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Vijana na Michezo ya Brunei

Nusu fainali ya mashindano hayo itafanyka Juni 11 na fainali imepangwa Juni 22.

Usajili unaweza kufanywa mtandaoni kwenye https://tinyurl.com/MTQBK-2023. Tarehe ya mwisho ya kujisajili ni Machi 27.

3482466

captcha