IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya 10 ya Qur'ani Ulaya yamepangwa kufanyika Hamburg, Ujerumani

14:35 - March 19, 2024
Habari ID: 3478539
IQNA – Mji wa Hamburg nchini Ujerumani utakuwa mwenyeji wa Awamu ya 10 ya Mashindano ya Qur'ani ya Ulaya mwezi ujao. Kituo cha Dar-ol-Qur'ani al-Kareem cha Ujerumani kinaandaa hafla hiyo ya Qur'ani.

Kulingana na tovuti ya Kituo cha Kiislamu cha Hamburg, mashindano hayo yamepangwa kufanyika Aprili 19-21, 2024.

Waislamu kutoka madhehebu zote za Kiisalmu wanaoishi Ulaya wanaweza kushiriki katika mashindano hayo katika vikundi viwili vya umri wa chini ya miaka 16 na 16 na zaidi katika sehemu mbili tofauti za wavulana na wasichana.

Usomaji wa Qur'ani au qiraa, kuhifadhi (katika viwango tofauti) na ufahamu wa Qur'ani ni kategoria za mashindano.

Katika kitengo cha ufahamu Qur'ani, wagombea watafanya mtihani wa kutafsiri Surah Al-Qamar.

Washindi watatu bora katika kila kitengo watapata zawadi za pesa taslimu kati ya euro 1,000 hadi 3,000.

Wawakilishi wa kila nchi ya Ulaya watakaopata alama za juu zaidi watatumwa kwenye mashindano ya kimataifa ya Qur'ani maeneo mengine duniani.

Tarehe ya mwisho ya kujiandikisha kwa ajili ya mashindano ya 10 ya Qur'ani ya Ulaya ni tarehe 9 Aprili.

Mashindano hayo ya kila mwaka yanalenga kukuza utamaduni na mafundisho ya Qur'ani, kubainisha na kukuza vipaji vya Qur'ani, na kuimarisha umoja katika wanaharakati wa Qur'ani Ulaya.

3487622

captcha