IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia Yamalizika, Washindi Watajwa

18:54 - August 24, 2023
Habari ID: 3477491
KUALA LUMPUR (IQNA) - Jopo la majaji wa shindano la 63 la kimataifa la Qur'ani la Malaysia lilitangaza washindi wa toleo hili la shindano hilo.

Sherehe ya kufunga mashindano hayo, inayojulikana rasmi kama Mkutano wa Kimataifa wa Kusoma na Kuhifadhi Qur'ani ya Malaysia (MTHQA), ilifanyika hapa katika mji mkuu wa Malaysia siku ya Alhamisi.

Kulingana na jopo la majaji, mwakilishi wa nchi mwenyeji alinyakua tuzo ya juu katika kitengo cha kusoma Qur'ani Tukufu.

Mwakilishi wa Iran Alireza Bijani, ambaye alitazamiwa kushinda tuzo ya juu katika kitengo hiki, alimaliza wa pili na mwakilishi wa Brunei akaibuka wa tatu.

Jumla ya wawakilishi 76 kutoka nchi 52 walishindana katika kategoria mbili za usomaji na kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika sehemu tofauti kwa wanaume na wanawake.

Wanaume 24 na wanawake 12 walishindana katika kitengo cha usomaji nyakati za jioni, na wanaume 27 na wanawake 13 katika kitengo cha kukariri kilichofanyika asubuhi.

Mashindano hayo yalirushwa moja kwa moja katika akaunti za mitandao ya kijamii za Idara ya Maendeleo ya Kiislamu Malaysia (JAKIM).

 4164744

Habari zinazohusiana
captcha