Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu amesema uzembe uliofanywa na serikali ya Saudi Arabia ndio uliosababisha tukio la maafa yaliyotokea katika mji mtukufu wa Makka.
2015 Sep 14 , 13:46
Jumapili ya jana msikiti mtakatifu wa al-Aqsa kwa mara nyingine tena ulivamiwa na Wazayuni waliojumuisha wanajeshi, polisi na Wazayuni wenye misimamo ya kufurutu ada ambapo damu za makumi ya Wapalestina zilimwagwa kiholela katika tukio hilo.
2015 Sep 14 , 13:35
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu za rambi rambi kufuatia ajali ya kusikitisha katika mji Mtakatifu wa Makka siku ya Ijumaa.
2015 Sep 13 , 12:39
Wafanyaziara wasiopungua 107 wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na kreni au winchi katika Msikiti Mtakatifu wa Makka, Saudi Arabia.
2015 Sep 11 , 23:34
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullahil-Udhma, Sayyid Ali Khamenei, amesema kuwa, Marekani haifichi uadui wake, na daima imekuwa ikipanga njama za kutaka kutoa pigo kwa taifa la Iran.
2015 Sep 10 , 12:06
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amezikosoa baadhi ya nchi za Ulaya kwa kufuata kibubusa sera za kiadui za Marekani kuhusiana na Iran.
2015 Sep 09 , 07:07
Maulamaa wa Kiislamu nchini Ghana wametangaza msimamo wa kupinga vikali kundi la kigaidi la Daesh au ISIS na kutoa wito kwa vijana nchini humo kuisoma na kufahamu ipasavyo tafsiri ya Qur'ani kwa njia sahihi ili wasitumbukie katika mtego muovu wa ISIS.
2015 Sep 08 , 16:18
Kongamano la kimataifa la "Uislamu, Rehema kwa Dunia" litafanyika Jakarta, Indonesia kuanzia Oktoba 13-16.
2015 Sep 08 , 12:41
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitizia ulazima wa kuweko mazalisho ya Kiislamu yenye umakini na mvuto kwa ajili ya kutumwa kwenye mitandao ya Intaneti.
2015 Sep 08 , 12:03
Mabudhha wenye misimamo mikali nchini Myanmar tayari wametangaza 'ushindi' dhidi ya Waislamu nchini humo katika uchaguzi utakaofanyika Novemba baada ya kupitishwa sheria tata dhidi ya Waislamu ambayo inawanyima Waislamu wa kabila la Rohingya haki ya kupiga kura.
2015 Sep 07 , 12:54
Katika jitihada za kupunguza ongezeko la ubaguzi na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu huko Malawi, jamii ya Waislamu nchini humo imeanzisha jitihada za kuwezesha vyombo vya habari kupata maelezo sahihi kuhusu Uislamu.
2015 Sep 07 , 11:03
Baraza la Maulamaa katika utawala wa Saudi Arabia wametangaza kuipinga filamu ya Mtume Muhammad SAW iliyotengenezwa Iran.
2015 Sep 06 , 12:05
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa, kupinga madola ya kibeberu duniani ni msingi wa Kiislamu.
2015 Sep 06 , 11:38