IQNA

Kongamano la "Uislamu, Rehema kwa Dunia" kufanyika Indonesia

12:41 - September 08, 2015
Habari ID: 3360473
Kongamano la kimataifa la "Uislamu, Rehema kwa Dunia" litafanyika Jakarta, Indonesia kuanzia Oktoba 13-16.

Kwa mujibu wa tovuti ya Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu, ICRO, tangazo kuhusu kongamano hilo limetolewa katika ufunugzi wa kikao cha An-Nahdhat al Ulamaa yaani Harakati ya Maulamaa mjini Jakarta.
Ugunuzi huo umehudhuriwa na Ma'rouf Amin mkuu wa baraza la utendaji la An-Nahdhat al Ulamaa, Aqeel Siraj mwenyekiti wa harakati hiyo, spika wa bunge la Indonesia pamoja na wabunge kadhaa, wanazuoni, mabalozi wa nchi mbali mbali na mkuu wa Idara ya Utamaduni ya Iran nchini Indonesia.
Akizungumza katika ufunguzi wa maonyesho yaliyofanyika pambizoni mwa kikao hicho, Haj Mansour Ramli ambaye ni katibu mwandalizi wa Kongamano la "Uislamu, Rehema kwa Dunia"  amesema mkutano huo unaleng akuarifisha Uislamu kama rehma kwa dunia.
Ameongeza kuwa katika kongamano hilo pia kutakuwa na warsha mbili zenye anuani za "Kuimarisha Mfumo wa Kiislamu wa Kifedha na Kiuchumi Duniani" na "Ugaidi Unaharibu Dini ya Kiislamu ambayo ni Rehema kwa Dunia". Amesema kongamano hilo limeandaliwa kufuatia muongozo wa Rais Jokowi wa Indonesia ambaye amesisitiza umuhimu wa mfumo wa Kiislamu wa kifedha katika kukabiliana na ugaidi na misimamo mikali. Ramli amesema kongamano hilo linalenga kusisitiza umuhimu wa dunia isiyo na ghasia na vita na ambayo ni sehemu salama na yenye amani kuishi watu wote sambamba na kuimarisha nafasi ya misikiti katika zama hizi za utandawazi. Wasomi Wairani walioalikwa katika kikao hicho ni pamoja na Muhammad Hassan Zamani na Sheikh Mesbahi Muqqadam.../mh

3358912

captcha