IQNA

Jinai za Israel

Iran: Mwisho wa 'Janga' kwa Wapalestina Unakaribia

21:40 - April 28, 2023
Habari ID: 3476928
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran anasema ukombozi wa Palestina na mwisho wa hali ya janga ambalo Wapalestina wanakabiliwa nalo unakaribia kwani utawala wa Kizayuni wa Israel unaonekana kuwa dhaifu kuliko hapo awali.

Nasser Kana'ani alitoa matamshi hayo katika taarifa kupitia ukurasa wake wa Twitter siku ya Ijumaa kabla ya kumbukumbu chungu ya siku ya kuundwa utawala haramu na bandia wa Israel ya Israeli, inayojulikana miongoni mwa Wapalestina kama siku ya Nakba, au janga.

"Licha ya kukandamiza taifa la Palestina kwa miaka 75, utawala wa ubaguzi wa rangi wa Israel unakabiliwa na mgawanyiko, kuzorota ndani, mgogoro wa utambulisho, na hivyo tunakaribia siku ya mwisho wa janga na ukombozi wa Palestina."

Kana'ani alisema Israel sio serikali ya kidemokrasia bali ni jeshi vamizi ambalo limekalia ardhi ya Palestina kwa mabavu.

"Kinyume na kile Wazayuni na wafadhili wao wa Magharibi wanasema, Israeli sio serikali ya kidemokrasia iliyoundwa katika ardhi isiyo na taifa, lakini ni jeshi vamizi ambalo limetawala ardhi ya taifa lingine na kuunda serikali ya kikabila na ya kibaguzi."

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia amesema madola ya Magharibi yalikuwa na nafasi kubwa katikauundaji na kubakia hai utawala haramu Israel, akisema madola ya Magharibi yanapaswa kuaibika kutokana na hali ya janga ambayo Wapalestina wanakabiliwa nayo.

"Ni aibu kuwa tawala za Marekani na Ulaya zilihusika katika kuunda utawala wa kibaguzi  rangi, na kupuuza uhalifu pamoja na ukiukaji wa haki za kibinadamu uliofanywa na utawala huu ghasibu na zimesimama pamoja mnyanyasaji na dhidi ya waliokandamizwa."

Siku ya Nakba huangukia Mei 15 kila mwaka, kuashiria kipindi ambacho utawala haramu wa Israel uliwafukuza mamia ya maelfu ya Wapalestina kutoka nyumba zao na kuwafungulia njia kwa walowezi wa Kizauni kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina miaka 75 iliyopita.

Wapalestina na waungaji mkono wao kote ulimwenguni huandaa mikutano na hafla mbali mbali katika Siku ya Nakba.

3483350

Kishikizo: nakba palestina israel iran
captcha