IQNA

Jinai za Israel

Mpalestina Khader Adnan amekufa shahidi akiwa ndani ya gereza la utawala wa Israel

16:54 - May 02, 2023
Habari ID: 3476945
TEHRAN (IQNA)- Wizara inayoshughulikia masuala ya Wapalestina wanaoshikiliwa mateka na walioachiwa huru imetangaza kuwa Sheikh Khader Adnan, mfungwa Mpalestina amekata roho na kufa shahidi ndani ya gereza la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Adnan, mmoja wa viongozi wa harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina, alikamatwa na utawala wa Kizayuni Februari 5 na kuamua kususia kula kwa muda wa siku 86 mfululizo akipinga kuwekwa kizuizini kiidara.

Sheria ya uwekaji kizuizini kiidara inatoa ruhusa kwa Wazayuni kumshikilia mtu kwa muda usiojulikana bila kumfungulia mashtaka. Kwa mujibu wa taasisi zinazofuatilia hali na matibabu ya wafungwa, wafungwa wapatao 500 kati ya takriban wafungwa 4,900 walioko kwenye magereza ya Israel wanashikiliwa kwa kutumia sheria hiyo.

Mahakama ya kijeshi ya utawala dhalimu wa Kizayuni wa Israel imekataa mara kadhaa kumwachia huru kwa dhamana Sheikh Khader Adnan ili akapatiwe huduma za matibabu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iranpress, Wizara inayoshughulikia masuala ya Wapalestina wanaoshikiliwa mateka na walioachiwa huru imetangaza leo asubuhi kuwa Sheikh Adnan amekufa shahidi ndani ya seli aliyokuwa amewekwa katika jela za utawala wa Kizayuni baada ya siku 86 za kususia kula.

Kabla ya hapo duru za habari ziliripoti kuwa Sheikh Khader Adnan amedhofu mno kiafya akiwa katika siku ya 85 ya mgomo wake wa kususia kula katika jela za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Wiki iliyopita, Adnan alipelekwa hospitalini baada ya hali yake ya kimwili kuwa mbaya zaidi, lakini utawala wa Kizayuni haukumruhusu wakili yeyote, madaktari au wanaohusika na masuala ya kisheria wawasiliane naye na kupata taarifa juu ya hali yake ya kiafya.

4137909

captcha