IQNA

Jinai za Israel

Binti shujaa Mpalestina ajibu jinai za utawala wa Kizayuni, afa shahidi

22:55 - May 05, 2023
Habari ID: 3476959
TEHRAN (IQNA)- Binti mmoja wa Palestina ametekeleza operesheni ya kishujaa ya kujitoa kufa shahidi ili kujibu jinai za mtawalia za wanajeshi makatili wa Israel na walowezi wa utawala huo pandikizi.

Mapema jana Alkhamisi asubuhi, tarehe 4 Mei, 2023, jeshi la utawala wa Kizayuni lilitangaza kuwa limewaua shahidi wanamapambano wawili wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS wanaojulikana kwa majina ya Hassan Qatani na Muadh al Masri wakiwa pamoja na Ibrahim Jabri, Mpalestina mwingine aliyewasaidia wanaharakati hao wawili wa HAMAS kupata sehemu ya kujificha. Wanamapambano hao wa Palestina walifanya operesheni ya kishujaa ya Al-Āghwār na kuangamiza walowezi watatu wa Kizayuni takriban mwezi mmoja uliopita. Majibu kutoka kwa wanamapambano wa Palestina dhidi ya Wazayuni yametolewa katika kipindi kifupi mno mara baada ya jeshi la Israel kufanya jinai ya kuwaua shahidi wanaharakati hao watatu wa Palestina, kinyume na ulivyotarajia utawala wa Kizayuni. Vyombo vya habari vya Kizayuni vimetangaza kuwa, binti mmoja Mpalestina mwenye umri wa miaka 26 amelipiza kisasi cha jinai hiyo ya Wazayuni ingawa na yeye mwenyewe amejeruhiwa kwa risasi na muda mfupi baadaye amekufa shahidi.

Operesheni hiyo ya kishujaa ya binti huyo wa Kipalestina ina nukta kadhaa za kutiliwa maanani.

Kwanza operesheni hiyo imethibitisha kuwa jinai yoyote ya Wazayuni haiwezi kuachwa vivi hivi bila ya kujibiwa na taifa shujaa la Palestina. Jengine ni kuwa majibu kwa jinai hizo za Wazayuni hayawahusu wanaume tu bali hata wanawake Wapalestina ni jinamizi kwa utawala mtenda jinai wa Kizayuni.

Vile vile operesheni hiyo ya binti wa Kipalestina imethibitisha kuwa, Wapalestina wote wanakubaliana kwa kauli moja juu ya wajibu wa kujibiwa jinai zote za Wazayuni. Msimamo huo ni jinamizi jingine kwa serikali yenye misimamo mikali kupindukia inayoongozwa na Benjamin Netanyahu huko Tel Aviv.

Suala jingine ni kwamba, operesheni hiyo ya binti wa Palestina inaonesha kuwa, Wapalestina wanao uwezo wa kujibu jinai za Wazayuni haraka sana, kadiri inavyowezekana. Wazayuni walifanya jinai ya kuwaua shahidi wanaharakati hao watatu wa Palestina jana asubuhi huko Nablos, jioni ya jana hiyo hiyo, binti huyo wa Kipalestina ameendesha operesheni ya kujibu jinai hiyo ya Wazayuni. Majibu hayo ya haraka sana ni uthibitisho kuwa Wapalestina wako tayari kwa lolote na muda wote. Ni uthibitisho pia kwamba, mapambano ya ukombozi wa Palesitna pamoja na makundi ya muqawama kama Hamas, Jihad al Islami na mengineyo, yanaungwa mkono vilivyo na wananchi wa Palestina.

4138634

captcha