IQNA

Kundi la Daesh limepotosha sura ya Uislamu na Waislamu

20:03 - September 15, 2014
Habari ID: 1450406
Mufti wa Quds na Ardhi za Palestina Sheikh Muhammad Hussein amesema kuwa kundi la kigaidi la Daesh limefanya matendo yanayopotosha sura ya Uislamu na ni tishio kwa Umma wa Kiarabu na Waislamu.

Sheikh Muhammad Hussein amesema kuwa kundi hilo linafanya vitendo kwa kutumia jina la Uislamu ambavyo ni kinyume kabisa na mafundisho ya dini hiyo.
Mufti wa Quds ameongeza kuwa, kundi hilo la kigaidi linapandikiza mbegu za fikra potofu za kidini na kisiasa katika umma wa Kiarabu na Kiislamu na kwamba kila mtu anayeliunga mkono kundi hilo ni adui wa Uislamu.
Sheikh Hussein amewataka Waislamu kurejea kwenye marejeo tajiri ya kidini na kiitikadi na kusisitiza kuwa, iwapo Umma wa Kiislamu unataka kuanzisha harakati adhimu kwa ajili ya kulinda dini na thamani zake unapaswa kurejea kwenye vyanzo asili vya Kiislamu na kuzuia mifarakano.
Mufti wa Quds ametahadharisha kuhusu hatua za Daesh za kuzusha hofu na kuchafua sura ya Uislamu na amewataka Waislamu kuwa macho mbele ya njama za kundi hilo za kugawa na kuzusha hitilafu katika Umma.  

1449696

Kishikizo: quds daesh kiislamu
captcha