Katika mahojiano na televisheni ya BNT Nickolay Mladenov amesmea kundi la kigaidi na kitakfiri la ISIS haliwezi kuangamizwa pasina kuwepo muungano wa kimataifa wa kijeshi.
Akiashiria hali ya mambo nchini Syria amesema: "Udiplomasia na maamuzi ya kisiasa ndio njia pekee inayofaa kumaliza mapigano katika nchi hii inayokumbwa na vita."
Nickolay Mladenov aidha amegusia hali ya mambo ya wakimbizi Waislamu na sera za baadhi ya nchi kuhusu suala hilo na kusema: "Zinapaswa kuchukuliwa hatua ili wahamiaji wapewe hifadhi katika maeneo yaliyo karibu na nchi zao ili hali ikiboreka warejee haraka."
Mladenov pia ametoa wito kwa nchi za Ulaya kutenganisha baina ya wakimbizi wanaokimbia vita na wale wanaotafuta ajira katika bara hilo.../mh