IQNA

Ayatullah Ahmad Khatami

Magaidi wa ISIS hawana uhusiano na Uislamu, ni mamluki wa Wazayuni

9:06 - November 21, 2015
Habari ID: 3454898
Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa wiki mjini Tehran amesema kundi la kigaidi la Daesh au ISIS matakfiri kwa ujumla ni mamluki wa Wazayuni ambao wametumwa kwa lengo la kuwagombanisha Waislamu.

Ayatullah Ahmad Khatami amesema hayo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya kisiasa na kimaanawi ya Swala ya Ijumaa mjini Tehran na kuongeza kuwa hakuna uhusiano wowote uliopo baina ya ugaidi na dini tukufu ya Kiislamu na kwamba, makundi ya kigaidi na kitakfiri kama Daesh yamekuja kwa lengo la kuifanya dini ya Kiislamu iogopwe na jukumu lao sio jingine ghairi ya kuichafulia jina dini hii tukufu.
Amesema kuwa, ili eneo la Mashariki ya Kati na ulimwengu kwa ujumla ushuhudie amani kuna haja ya kuweko ushirikiano wa kweli na wa dhati wa nchi zote katika suala zima la kupambana na ugaidi. Sambamba na kulaani mashambulio ya kigaidi ya hivi karibuni mjini Paris Ufaransa, Ayatullah Khatami amesisitiza kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapinga mauaji dhidi ya watu wasio na hatia na inaamini kwamba, njia pekee ya kung’oa mizizi ya tishio la ugaidi na hatari yake kwa ulimwengu ni kuweko muungano wa kweli na wa nchi zote kwa ajili ya kupambana na tatizo hilo.
Kadhalika amekosoa siasa za kindumakuwili za madola ya Ulaya na Marekani katika suala la ugaidi na hatua yao ya kuugawa katika makundi mawili ya ugaidi mzuri na mbaya. Amesema, madola hayo yameghadhibishwa na ugaidi wa hivi karibuni huko Paris Ufaransa lakini yamekuwa hayaonyeshi radiamali yoyote kwa mauaji ya kila leo ya Israel dhidi ya Wapalestina na hata yamenyamazia kimya mashambulio ya kigaidi ya hivi karibuni huko Beirut Lebanon.

3454724

captcha