IQNA

Wapalestina kuandamana 'Ijumaa ya Ghadahbu' kulaani Israel

9:59 - December 11, 2015
Habari ID: 3462045
Wapalestina hii wanashiriki katika maandamano makubwa yaliyopowa anuani 'Ijumaa ya Ghadhabu' ilikulaani jina za utawala haramu wa Israel na kuunga mkono mapambano na intifadha au mwamko dhidi ya utawala huo.

Imearifiwa kuwa makundi mbali mbali ya kupigania ukombozi Palestina yakiwemo ya kitaifa, Kiislamu na vijana yametoa wito kwa Wapalestina wote kujitokeza katika maandamano yanayofanyika maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Ghaza. Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina Hamas imetoa taarifa na kuwataka Wapalestina wajitokeze kwa wingi katika maandamano ya leo.
Taarifa hiyo imesema, maandamano hayo yatafanyika kulaani utawala haramu wa Israel, kuunga mkono Intifadha (mwamko) ya Quds na pia kuadhimisha kuundwa Hamas.
Machafuko mapya katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu yalianza baada ya utawala haramu wa Israel kuwazuia Waislamu wa Palestina kuingia katika Msikiti Mtakatifu wa al Aqsa mwezi Agosti mwaka huu.
Wapalestina zaidi ya 120 wakiwemo wanawake na watoto wameuawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel tokea mwanzo wa mwezi wa Oktoba, ilipoanza Intifadha 3.

3462036

captcha