IQNA

Utawala wa Bahrain wazidi kuwakandamiza wanazuoni wa Kiislamu

0:29 - August 08, 2016
Habari ID: 3470504
Utawala wa kifalme Bahrain umeendeleza ukandamizaji wa wanazuoni mashuhuri wa Kiislamu, katika fremu ya kampeni dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo.

Utawala wa Bahrain wazidi kuwakandamiza wanazuoni wa Kiislamu

Miongoni mwa waliokamatwa katika wimbi jipya la kamatakamata ya polisi ya Bahrain ni Sheikh Issa Momen, Imam wa Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Khayf katika kitongoji cha Dair, mashariki mwa mji mkuu Manama.

Shakhsia wengine wa Kiislamu waliokamatwa na polisi ya Bahrain ni Sheikh Ali al-Hamli, Sayyid Mohsen Qarifi na Sheikh Fazil Zaki waliokamatwa mashariki mwa mji wa Manama.

Agosti Pili, Maulamaa wa Bahrain akiwemo Sheikh Issa Qasim na Sayyid Abdullah al-Ghuraibi walitoa taarifa na kuwataka viongozi wa utawala wa Aal-Khalifawamwachilie huru Sayyid Majid al-Mash'al, Mkuu wa Baraza la Maulamaa wa Kiislamu la nchi hiyo pamoja na shakhsia wengine wa kidini na wasio wa kidini walioko kwenye jela za utawala huo. Vikosi vya usalama vya utawala wa Aal Khalifa, asubuhi ya tarehe 30 Julai viliivamia nyumba ya Sheikh Majid al-Mash'al na kumtia nguvuni alimu huyo wa Kishia bila ya kumueleza sababu wala tuhuma zinazomkabili.

Malalamiko na maandamano ya wananchi wa Bahrain dhidi ya watawala dhalimu wa nchi hiyo yamekuwa yakiendelea tokea tarehe 14 Februrai 2011. Tokea mwanzoni mwa maandamano hayo watawala wa ukoo wa Aal Khalifa wamekuwa wakitekeleza mbinu tofauti za kupambana na wapinzani.

3460617

Kishikizo: bahrain iqna kiislamu
captcha