Molavi Abdol-Hamid Ismail-Zahi, Imam wa Sala ya Ijumaa wa Ahul Sunna katika mji wa Zahedan ameashiria Hadithi ya Mtume Mtukufu alisema wakati ugonjwa wa tauni unapoenea katika eneo, wakaazi hawapaswi kuondoka eneo hilo na wengine hawapaswi kuingia katika eneo hilo kwani kufanya hivyo kutapelekea ugonjwa huo kuenea zaidi.
Akihutubia wanafunzi leo katika Chuo cha Darul Uluum mjini Zahedan amesema: "Uislamu si dini ya nadharia bali ni dini ya vitendo."
Aidha amesema Sira ya Mtume SAW ina uwezo mkubwa wa kutumia katika maisha.
Akizungumzia kirusi cha Corona amesema: "Imearifiwa kuwa kirusi cha Corona pia kimefika katika nchi yetu na baadhi wameambukizwa katika baadhi ya mikoa." Molavi Abdol-Hamid IsmaIl-Zahi ametoa wito wa kutekelezwa ushauri wa Mtume SAW kuhusu magonjwa ambukuzi na pia amewataka wananchi wasiingiwe na hofu kubwa na watawakali kwa Mwenyezi Mungu SWT.