IQNA

Katibu Mkuu wa UN atahadharisha kuhusu kukandamizwa Waislamu wakati wa COVID-19

22:34 - May 08, 2020
Habari ID: 3472746
TEHRAN (IQNA) – Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema janga la COVID-19 au corona limeibua 'tsunami ya chuki' na hivyo ametoa wito wa kusitishwa matamshi yaliyojaa chuki duniani.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kumeenea hisia dhidi ya raia wa kigeni katika mitandao na katika mitaa huku kukishuhudiwa hujuma dhidi ya Waislamu ambazo zinahusiana na janga la COVID-19.

Gutterres amesema wahajiri na wakimbizi wamelaumiwa visivyo kuwa ndio chanzo cha COVID-19 na wamenyimwa huduma za afya. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa vyombo vya habari na wasimamizi wa mitandao ya kijamii kuondoa chochote kile kinachoibua ubaguzi na chuki.

Katika wiki za hivi karibuni kumeshuhudiwa chuki dhidi ya Waislamu kwa msingi wa COVID-19 ambapo Waislamu nchini India hasa wameripoti kesi nyingi za ubaguzi na ukandmizaji.

Idadi ya walioambukizwa corona duniani kote hadi sasa ni zaidi ya milioni 4 ambapo watu wasiopungua 270,000 wameaga dunia na wengine zaidi ya milioni moja na laki tatu wametibiwa na kupata nafuu. 

3897256/

captcha