IQNA

Wapalestina 50,000 washiriki katika Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al-Aqsa

9:17 - June 06, 2020
Habari ID: 3472840
TEHRAN (IQAN)- Swala ya Ijumaa imeswaliwa katika Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) kwa mara ya kwanza jana baada ya msikiti huo kufungwa kwa wiki kadhaa kutokana na janga la COVID-19.

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Wakfu wa Kiislamu katika mji wa Quds, zaidi ya waumini 50,000 walishiriki katika Swala ya Ijumaa jana.

Maafisa wa msikiti huo wanasema waumini walijitahidi kuzingatia kanuni za afya wakati wa swala huku waumini wakipewa barakoa na sanitaiza kabla ya kuingia msikitini.

Idara ya Wakfu wa Kiislamu katika mji wa Quds iliufunga Mskiti wa Al-Aqsa mwezi Machi kwa lengo la kuzuia kuenea COVID-19.

Msikiti huo umefunguliwa kwa mashauriano na wakuu wa sekta ya afya na wote wanaofika msikitini hapo wanatakiwa kuzingatia kanuni za afya zilizowekwa.

3903073

captcha