IQNA

Qarii Taruti wa Misri akisoma aya katika Sura al-Furqan + Video

17:31 - December 07, 2020
Habari ID: 3473431
TEHRAN (IQNA) – Hivi karibuni qarii mashuhuri wa Misri Sheikh Abdul Fattah Taruti alishiriki katika kikao ambacho alisoma aya moja katika Sura al-Furqan ya Qur'ani Tukufu.

Katika klipu ambayo imeenezwa katika mitandao ya kijamii na Kituo cha Darul Qur'an cha Ujerumani, Taruti anasema aya ya 61 ya Sura al Furqan isemayo: "Ametukuka aliye zijaalia nyota mbinguni, na akajaalia humo taa na mwezi unao ng'ara."

Sheikh Taruti alizwaliwa mwaka 1965 katika kijiji cha Tarut karibu na mji wa Zagazig jimboni Sharqia. Alianza kuhifadhi Qur’ani akiwa na umri wa miaka mitatu na alifanikiwa kuhifadhi Qur’ani kikamilifu akiwa na umri wa miaka 8. Taruti alisoma katika tawi la Zagazig la Chuo Kikuu cha Al Azhar na aliendelea  kuimarisha uwezo wake wa Qur’ani kwa kupata mafunzo kwa kutoka kwa wasomi wakubwa kama vile Sheikh Mohammad Al-Lithi, Shahat Anwar and Saeed Abdul Samad.

3939276

Kishikizo: taruti qarii misri
captcha