IQNA

TV Qur’an ya Iran yarusha hewani qiraa ya Qur’ani ya wasomaji mashuhuri wa Misri

12:16 - January 10, 2021
Habari ID: 3473542
TEHRAN (IQNA)- Televisheni ya Qur’ani ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) imezindua kipindi kipya cha kurusha hewani qiraa ya Qur’ani Tukufu ya wasomaji maarufu wa Misri.

Kwa mujibu wa  mwandishi wa IQNA,  kipindi hicho kilianza Jumamosi usiku kwa qiraa ya Qur’ani Tukufu ya  Sura Nazi’at na Fajr ya Shahat Mohammad Anwar na  leo usiku watazamaji  wataweza kuona qiraa ya Sura al Muzzamil na Qiamah  ya Mohammad Ahmad Shabeeb.

Aidha Januari 11 televisheni hiyo ya Qur’ani ya Iran itarusha hewani kwa mara ya kwanza qiraa ya Surah Naba, Tariq na Alaq ya  Ustadh Ghalwash.

Televisheni ya Qur’ani ya Iran mara kwa mara hurusha hewani qiraa ya wasomi mashuhuri wa Misri.

3946648

captcha