Abdullah anayeishi katika kijiji cha Tal al Jarad katika jimbo la Sharqia alianza kusoma Qur’ani mwaka 2014 chini ya Ustadh Mohamad Hassan Alwan. Baada ya miezi mitatu tu alifanikiwa kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu na baada ya hapo akaweza kuhitimu katika kusoma Qur’ani kwa mbinu 10 tafauti.
Alwan pia ana uwezo wa kufasiri aya zote za Qur’ani kwa lugha za Kifaransa na Kiingereza.
Kijana huyo ameweza kushinda mashindano kadhaa ya kimkoa, kitaifa na kimataifa ya Qur’ani Tukufu. Mwaka 2018 alifanikiwa kushinda mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Misri.
Kijana huyo ameenziwa mara mbili na Rais Abdel Fattah el Sisi kutokana na mafanikio yake katika kuhifadhi Qur’ani Tukufu.