Uamuzi huo wa UNESCO umekuja baada ya pendekezo la nchi 15 za Kiislamu ambazo mwaka ujao zitawasilisha ripoti zikibainisha hatua zilizochukuliwa kuimarisha sanaa hiyo ya kaligrafia ya Kiislamu na Kiarabu.
Kaligrafia ya Kiarabu ni mtindo wa kipekee wa kuandika maandish ya Kiarabu yenye mvuto wa aina yake.
Orodha ya Turathi za Kiutamaduni za Mwanadamu ilianzishwa mwaka 2008 na hujumuisha masuala ya kiutamaduni. Katika miaka ya hivi karibuni orodha hiyo imejumuisha mizik, densi, michezo na tamasha na pia vyakula.