IQNA

Msikiti wahujumiwa Vienna, Austria

21:44 - February 05, 2022
Habari ID: 3474893
TEHRAN (IQNA)- Msikiti mmoja katika mji mkuu wa Austira, Vienna umehujumiwa na watu wasiojulikana ikiwa ni ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya.

Taarifa zinasema Msikiti wa Ebubekir umelengwa na wafuasi wa kundi la kigaidi la PKK. Kundi hilo pia hivi karibuni lilishambulia Msikiti wa Jamia wa Jumuiya ya Utamaduni wa Kiislamu ya Turkey-Austria.

Balozi wa Uturuki nchini Austria Ozan Ceyhun amebainisha masikitiko yake kufuatia shambulizi hilo ambalo limejiri katika usiku mtakatifu wa Laylat al Raghaib, ambao ni usiku wa kwanza wa Mwezi wa Rajab.

Amesema klipu ya video ya shambulizi dhidi ya msikiti huo imekabidhiwa wakuu wa usalama na inatazamiwa kuwa wahalifu waliohusika watakamatwa.

Waziri wa Ujumuishaji Austria na wanasiasa wengine wamelaani hujuma dhidi ya misikiti na wamesisitiza kuhusu umuhimu wa uhuru wa kuabudu.

Faika el Negashi, msemaji wa Chama cha Kijana amesema hujuma dhidi ya msikiti ni  hujuma dhidi ya demokrasia na uhuru.

Mwaka jana Waziri wa Utangamano wa Austria, Susanne Raab alizindua tovuti inayoitwa Ramani ya Kitaifa ya Uislamu, ambayo ina majina na maeneo ya misikiti, jumuiya, na maafisa zaidi ya 620 Waislamu na mawasiliano yao nje ya nchi.
Taarifa hiyo imesema: "Ni muhimu kwa Austria kuacha kulenga wahamiaji na Waislamu kwa kuwatia "alama", na badala yake itekeleze sera za kuwajibika".

Hatua hiyo ililaaniwa vikali na kutajwa kuwa ni njama ya kuwabana Waislamu.

/3477682

Kishikizo: austria waislamu msikiti
captcha