Apu hiyo ambayo imepewa juna la "Qur'ani Sahbi' (Qurani ni Sahaba Wangu) imeundwa na Jumuiya ya Misaada ya Kuwait kwa ajili ya Huduma kwa Qur'ani Tukufu.
Tayari maelfu ya Waislamu wameshaanza kuitumia apu hiyo ili waweze kunufaika nayo. Afisa mwandamizi wa jumuiya hiyo Ahmed al Murshid amesema apu hiyo inmsaidia mtu kusoma Qur'ani binafsi, au pamoja na jamaa na marafiki.
Aidha inahesabu kila herufi inayosomwa kama njia ya kukumbusha Hadithi ya Mtume Muhammad SAW isemayo kuwa kila anayesoma herufi katika Qur'ani Tukufu, Allah SWT anampa thawabi 10.
Al Murshid anasema wanaotaka kuipata apu hiyo wanaweza kuipata kupitia majukwaa ya Google Play Store, Apple Store au katika tovuti ya hofath.org