IQNA

Umrah

Waumini milioni 22 watembelea Msikiti Mkuu wa Makka katika Siku 20 za Kwanza za Ramadhani

18:39 - April 14, 2023
Habari ID: 3476866
TEHRAN (IQNA) – Zaidi ya waumini milioni 22 walitembelea eneo takatifu zaidi katika Uislamu, Msikiti Mkuu Makka (Masjid al-Haram) katika siku 20 za kwanza za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.

Haya yalitangazwa na Idara ya Mkuu wa Masuala ya Masjid al-Haram na Msikiti wa Mtume (Al Masjid An Nabawi).

Abdulrahman bin Abdulaziz Al-Sudais idadi hiyo imeweza kufikiwa kufuatia mkakati wa kina wa operesheni ili kuhakikisha idadi kubwa ya waumini na wanaweza kutembelea eneo hilo takatifu kufanya ibada zao kwa urahisi, Shirika rasmi la Habari la Saudi (SPA) liliripoti.

Ramadhani, iliyoanza Machi 23, imeshuhudia wimbi kubwa la wanaoshiriki katika ibada ya Hija ndogo ya Umrah katika maeneo matakatifu nchini Saudi Arabia.

Wakati huo huo, vyombo vya habari vya Saudi vinaripoti kwamba mpango ambao unalenga kuwarahishia waumini katika siku za mwisho za Ramadhani na kuhakikisha huduma za ubora wa juu zilianza kutekelezwa Jumanne.

Mpango huo unajumuisha kuosha Msikiti Mkuu mara 10 kwa siku katika zoezi litakalosimamiwa na wafanyakazi zaidi ya 4,000 ambapo kuna timu zaidi ya 70 pia zinazofanya kazi usiku na mchana kusafisha maeneo yote ya msikiti.

Teknolojia za Akili ya Mashine (AI) pia zitatumika kutekeleza shughuli kusafisha Al Masjid Al Haram ili kuhakikisha kuwa hakuna virusi vyovyote katika eneo hilo takatifu.

Mpango huo pia unatoa takriban magari 8,000, yakiwemo 3,000 ambayo ni ya umeme, ili kuwasafirisha waumini kutoka sehemu za kuegesha magari hadi kumbi za sala. Waumini wanaweza kujisajili kutumia magari hayo  mapema kupitia programu ya Tanaqol.

Zaidi ya wafanyikazi 160 watawekwa kwenye milango ya Msikiti Mkuu ili kuwezesha waumini kuingia na kutoka na kujibu maswali yoyote.

Abdulaziz Al-Sudais aliwataka wote wanaofika katika AL Masjid Al Haram kuzingatia maagizo yote na kubainisha kuwa ushirikiano na walinda usalama ni muhimu ili kudumisha ulinzi na usalama.

3483194

captcha