IQNA

Shughuli za Qur'ani

Kijiji cha Misri ambacho familia zote zina angalau mmoja wao aliyehifadhi Qur'ani

16:20 - May 27, 2023
Habari ID: 3477053
TEHRAN (IQNA) - Matar Tares ni jina la kijiji ambapo familia zote zina kumbukumbu moja ya Quran nzima.

Kijiji hicho kiko karibu na Sinnuris, jiji lililo katika Jimbo la Faiyum katikati mwa nchi.

Miaka iliyopita Maktab (shule ya kijadi ya Qur'ani) ilizinduliwa kijijini hapo na tangu wakati huo, idadi ya wale wanaojifunza Kitabu Kitakatifu kwa moyo imekuwa ikiongezeka.

Kila familia katika kijiji hiyo ina mwanafmailia angalau moja aliyehifadhi Qur'ani Tukufu n ahata kuna familia mbazo wanafamilia wote wamehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Hivi sasa, kijiji cha Matar Tares kina zaidi ya wahifadhi 20,000 wa Qur'ani, kulingana na Watan daily.

Sheikh Ahmed Mohamed Yusuf, mwanakijiji, anasema kuna aina fulani ya ushindani mwema kati ya familia ili kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

Anasema watoto huanza kuhifadhi Qur'ani Tukufu wakiwa na umri wa miaka mitano na kukamilisha mchakato huo katika takriban miaka sita.

Ndiyo maana wengi wa wanafunzi wanaofika darasa la sita au miaka michache baadaye wamehifadhi Qur'ani nzima, anaongeza.

Pia anabainisha kuwa watoto katika kijiji hicho wameshinda mataji mengi katika mashindano ya Qur'ani katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Wanafaulu katika nyanja zingine pia, Sheikh Yusuf anasema.

Kila mwaka sherehe hufanyika kijijini hapo kwa ajili ya kuwaenzi wahifadhi Qur'ani na wanakijiji sasa wanajiandaa kwa tukio la mwaka huu.

Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100.

Waislamu wanachukua karibu asilimia 90 ya wakazi wote wa nchi hiyo ya Kiarabu, ambapo shughuli za Qur'ani ni za kawaida sana.

An Egyptian Village Where All Families Have At Least One Quran Memorizer

An Egyptian Village Where All Families Have At Least One Quran Memorizer

An Egyptian Village Where All Families Have At Least One Quran Memorizer

 

4143764

captcha