IQNA

Harakati za Qur'ani

Wasomaji Qur'ani Wairani wakiwa katika Jabal al Noor + Video

Makka (IQNA)Vijana wawili wasomaji Qur'ani Tukufu Wairani, ambao wamekwenda katika ardhi ya Wahyi (Makka) wakiwa katika msafara wa Qur'ani wa Noor, walishiriki katika mashindano ya aya za mwanzo za Surah Al-Alaq katika eneo la Pango la Hira.

Kwa mujibu wa IQNA, Mohammad Hosseinipour na Mohammad Mahdi Rouhani Sarostani, wajumbe wa msafara wa Qur'ani wa Noor, waliotumwa kwenye ardhi ya Wahyi, katika siku chache zilizopita, walisoma aya tano za mwanzo za Surah Al Alaq.

Ikumbukwe kuwa Seyyed Mohammad Hosseinipour alizaliwa Damghan mwezi Mei 1979 na hadi sasa ameorodheshwa katika mashindano mengi yakiwemo mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya wanafunzi wa ulimwengu wa Kiislamu katika fani ya usomaji mwaka 1996, na mashindano ya kitaifa. ya wanafunzi wa Wizara ya Sayansi mwaka 1998.

Mohammad Mahdi Rohani Sarvostani alizaliwa katika jiji la Sarvostan na ana shahada ya uzamili ya Kiingereza. Kwa sasa anafanya kazi kama mwalimu wa lugha katika chuo kikuu.

Tangu alipokuwa mwanafunzi, amekuwa akijihusisha na shughuli za Qur'ani na ameshinda mara kadhaa katika mashindano ya kitaifa na mikoani.

Kishikizo: hira ، qurani tukufu