IQNA

Turathi za Kiislamu

Maktaba ya Msikiti Mtakatifu wa Makka yaonyesha Misahafu ya kipekee

14:52 - July 08, 2023
Habari ID: 3477252
MAKKA (IQNA) - Maktaba ya Msikiti Mkuu wa Makka nchini Saudi Arabia inaonyesha Misahafu (Nakala za Qur'ani) ya kipekee ya kale na pia michoro ambayo ina aya za Qur'ani Tukufu.

Idara ya Maktaba na Masuala ya Kitamaduni ya Urais Mkuu wa Misikiti Miwili Mitakatifu inaonyesha Misahafu saba ya kale katika sehemu ya wanawake ya maktaba ya Msikiti Mkuu huko Makka.

Katika maonyesho hayo kuna Misahafu iliyoandikwa  wakati wa utawala wa Uthman bin Affan, picha za kuchora ambazo zina aya za Qur'ani za mwandishi Mohammed Ibrahim, na nakala adimu ya "Musnad Al-Muwatta," maandishi ya kwanza ya kisheria kujumuishwa Hadith na Fiqh.

Umaima binti Abdulrahman Al-Sudais, mkuu wa shughuli za wanawake katika idara hiyo, alisema kuwa jumba la makumbusho linalenga kutumika kama jukwaa la watu - kutoka watafiti hadi Mahujaji - kupanua maarifa yao ya kihistoria na kitamaduni.

Majumba ya makumbusho huko Makka yana vitu vya kale adimu ambavyo vina zaidi ya miaka 1,400, vinavyoangazia historia tajiri ya mahali hapo.

Wataalamu wanayachukulia majumba haya ya makumbusho kama lango la maarifa ambapo wageni hupata ujuzi muhimu kuhusu utamaduni na historia ya Makka.

3484246

captcha