IQNA

Kongamano la Kimataifa dhidi ya ugaidi Damascus, Syria

11:41 - July 25, 2015
Habari ID: 3332772
Mji mkuu wa Syria , Damascus ni ulikuwa mwenyeji wa kongamano la kimataifa la 'Vyombo vya Habari na Vita Dhidi ya Ugaidi.'

Katika kongamano hilo la siku mbili linalomalizika leo Jumamosi, makumi ya wasimamizi wa vyombo vya habari kutoka nchi za Kiarabu na zisizo za Kiarabu kama vile, Russia, Iran, Cuba, Uhispania, China, Misri, Afghanistan, Lebanon, Iraq, Algeria, Bahrain, Sudan, Tunisia, Cyprus, Ujerumani na Kuwait wameshiriki.
Washiriki katika kongamano hilo wamejadili nafasi ya vyombo vya habari vya kitaifa na binafsi katika vita vya kimataifa  dhidi ya ugaidi. Aidha wametathmini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika vita vya sasa duniani na pia katika mustakabali. Walid al Mualim Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amehutubu katika ufunguzi wa kikao hicho na kusema pamoja na kuwepo kile kinachotajwa kuwa ni 'muungano wa kimataifa' kwa lengo la kupambana na kundi la kigaidi la Daesh au ISIS, muungano huo haujafanikiwa  hata kidogo na kwamba ni wanajeshi wa Syria na wapiganaji wa Hizbullah ndio walioweza kukabiliana vilivyo na ugaidi wa Daesh.
Naye Wael Al Halqi Waziri Mkuu wa Syria amebainisha kuridhishwa kwake na ushiriki wa idadi kubwa wa jumbe za kimataifa katika kongamano hilo la Damascus. Ameelezea matumaini yake kuwa, kufanyika kongamano hilo ni ishara ya imani walionyao wajumbe hao kwa serikali na watu wa Syria. Aidha amesema kongamano hilo ni kiashirio cha nafasi muhimu ya vyombo vya habari katika vita dhidi ya ugaidi na misimamo mikali.
Wawakilishi wa Iran, China, Russia na nchi zingine kadhaa walipendekeza kuundwe taasisi moja kubwa ya habari kwa lengo la kuleta muungano wa kihabari katika vita dhidi ya ugaidi na utakfiri.
Kongamano la kimataifa la 'Vyombo vya Habari na Vita Dhidi ya Ugaidi limefanyika katika hali ambayo baadhi ya nchi zimebadilisha sera zao za kichochezi na kuingilia mambo ya Syria. Jambo hili ni ishara kuwa busara ya uongozi na mapambano ya Wasyria ni jambo ambalo limezaa matunda na kupelekea madola chokozi hayo yabadili sera  zao kuhusu Syria.
Baadhi ya wakuu wa nchi za Kiarabu na Magharibi akiwemo waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, hivi kairbuni alikiri kuwa nchi za magharibi hazitaki tena kuipindua serikali ya Syria.  Jitihada za hivi za Uingereza kutaka kufungua tena ubalozi wake mjini Damascus ni ishara mojawapo ya kubadilika sera za London. Pamoja na hayo, sambamba na kuendelea jitihada za kidiplomasia kutatua mgogoro wa Syria hasa kupitia Umoja wa Mataifa, kuna udharura kwa nchi zainazodai kupambana na ugaidi, na ambazo wakati huo huo zinaunga mkono magaidi, kusitisha himaya yao kwa magaidi na kuwazuia kuingia Syria.../mh

3332476

captcha