IQNA

Fikra za Qur'ani

Kongamano la Kimataifa la Fikra za Qur'ani za Ayatullah Khamenei

18:14 - December 20, 2023
Habari ID: 3478065
IQNA - Kongamano la Kuchunguza Fikra za Qur'ani za Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei.

Ofisi ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa huko Isfahan kati mwa Iran imeandaa hafla hiyo ya kielimu leo Jumatano, Disemba 20.

Hujjatula Islam Seyed Amir Reza Tahaei, mkuu wa ofisi hiyo alibainisha katika mkutano na waandishi wa habari amebainisha kuwa kongamano hilo ni la tatu baada ya matoleo mawili ya awali kufanyika Tehran katika miaka ya nyuma.

Kulingana na msomi huyo, zaidi ya makala 2,400 ziliwasilishwa kwa sekretarieti ya kongamano hilo.

Makala hizo zinazjumuisha 244 katika lugha 22 mbali mbali zilizoandikwa na wasomi na watafiti kutoka nchi 21, alisema.

Amesema vikao 183 vya awali vilifanyika katika mikoa 30 ya Iran kabla ya tukio kuu na kuongeza kuwa kumekuwa na warsha 65 pia.

Ameeleza matumaini yake kuwa kongamano hilo la kimataifa litasaidia kukuza utamaduni wa Qur'ani Tukufu katika jamii.

719362

Habari zinazohusiana
captcha