IQNA

UNESCO yakosoa sera za Israel za kukalia kwa mabavu Palestina

15:39 - May 03, 2017
Habari ID: 3470966
TEHRAN (IQNA)-Kamati ya Utendaji ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Utamaduni na Sayansi UNESCO Jumanne ilipitisha azimio ambalo liliulaani utawala wa Kizayuni wa Israel kwa ajili ya kukiuka sheria za kimataifa katika mji wa Quds (Jerusalem) na Ukanda wa Ghaza.

Azimio hilo aidha liliutaka utawala wa Kizayuni wa Israel uheshimu utambulisho wa kihistoria wa mji wa Quds.

Azimio hilo la UNESCO limetaja Israel kuwa "utawala ghasibu' na limeutaka utawala huo usitishe uchimbaji wake usio na kikomo na utengenezaji wa njia za chini kwa chini na miradi mingine  katika eneo la Mashariki mwa Quds Tukufu.

Azimio hilo limetolewa ikiwa inakaribia mwaka wa 69 wa kuundwa utawala bandia wa Israel ambao unakalia kwa mabavu ardhi za Palestina na Quds Tukufu, kibla cha kwanza cha Waislamu.

Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni wa Israel amekasirishwa mno na upasishwaji wa azimio hilo dhidi ya Israel katika UNESCO. Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel amedai kuwa azimio lililopasishwa na UNESCO ni  la udiplomasia wa kipuuzi,

Mwaka jana pia UNESCO ilipitisha azimio jingine ambalo lilitilia shaka uhusiano wa Uyahudi na maeneo matakatifu ya Quds jambo ambalo liliughadhibisha sana utawala wa Kizayuni. Kufuatia azimio hilo, utawala wa Kizayuni wa Israel ulisimamisha kwa muda uhusiano wake na UNESCO.

Hadi sasa UNESCO imepitisha maazimio kadhaa dhidi ya utawala wa Kizayuni na kuitaja Israel kuwa utawala ghasibu ambao unapaswa kutekeleza maamuzi ya kimataifa na maazimio ya UNESCO kuhusu turathi za kihistoria za Quds Tukufu eneo ambalo mwaka 1981 lilitembuliwa na UNESCO kama mojawapo ya turathi za dunia.

Kamati ya Utendaji wa UNESCO Aprili mwaka 2015 pia iIiushurutisha utawala ghasibu wa Israel uwazuie Wazayuni wenye misimamo ya kufurutu ada na wanajeshi wa Israel kuuvamia na kuvunjia heshima Msikiti wa Al Aqsa na Wapalestina.

3462739/


captcha