IQNA

Jinai za Israel

Kwa Ijumaa ya Kumi Mfululizo Israel yawawekea Wapalestina vizuizi katika Msikiti wa Al-Aqsa

7:10 - December 16, 2023
Habari ID: 3478040
IQNA - Maelfu ya Wapalestina hawakuweza kuhudhuria sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al-Aqsa mjini Quds (Jerusalem) kwa wiki ya kumi kutokana na vizingiti vilivyowekwa na utawala dhalimu wa Israel tangu kuanza kwa vita dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 7.

Afisa kutoka Idara ya Wakfu ya Kiislamu mjini Jerusalem alisema kuwa ni waumini 7,000 pekee walioingia msikitini, ikilinganishwa na 50,000 wa kawaida siku za Ijumaa za kawaida. Afisa huyo, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kuwa vikosi vya Israeli vilizuia makumi ya maelfu ya kuingia katika msikiti huo ambao ni eneo la tatu kwa utakatifu katika Uislamu.

Walioshuhudia walisema kwamba ni wazee wachache tu ndio waliweza kufika msikiti huo, ambao ulionekana kuwa na waumini wachache sana. Pia walisema kuwa polisi katili wa Israel waliwazuia na kuwashambulia vijana wa Kipalestina waliojaribu kufika katika Msikiti wa Al-Aqsa kupitia vichochoro vya Mji Mkongwe.

Mamia ya Wapalestina walilazimika kusali katika mitaa iliyo karibu na al-Quds inayokaliwa kwa mabavu, kama vile Mtaa wa Salah al-Din, Al-Musara, na Wadi al-Joz.

Zaidi ya Wapalestina 19,000 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wameuawa shahidi wakati wa vita vya mauaji ya halaiki ambavyo Israel ilivianzisha tarehe 7 Oktoba, kufuatia operesheni iliyofanywa na makundi ya muqawama ya Gaza iliyopewa jina la Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa.

3486430

Habari zinazohusiana
captcha