IQNA

Jinai za Israel

Tamko kali la Hamas baada ya Wazayuni kumuua kijana Mpalestina karibu na Msikiti wa al-Aqsa

17:00 - April 01, 2023
Habari ID: 3476796
TEHRAN (IQNA)-Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesisitiza kuwa, damu mashahidi wa Palestina italinda utambulisho wa Kipalestina, Kiarabu na Kiislamu wa msikiti mtakatifu wa al-Aqsa ulio katika mji wa Quds au Jerusalem.

Hazim Qassim akitoa radiamali yake kuhusiana na jinai za Wazayuni maghasibu amesema, hatua ya jeshi la Israel ya kumuua kwa kumpiga risasi kijana wa Kipalestina katika eneo la kuingia katika Msikiti wa al-Aqsa ni vita vya kidini vya utawala huo ghasibu dhidi ya taifa la Palestina na matukufu yake.

Ijumaa usiku wanajeshi wa Israel walimuua shahidi kwa kumpiga risasi kijana mmoja wa Kipalestina aliyekuwa akitaka kumlinda mwanamke wa Kipalestina aliyekuwa amevamiwa na wavamizi.

Msikiti wa Al-Aqsa, ikiwa ndio nembo kuu ya utambulisho wa Kiislamu na Kipalestina katika mji wa Baitul Muqaddas au Quds daima umekuwa ukiandamwa na hujuma na vitendo vya uharibifu vya utawala ghasibu wa Kizayuni.

Katika radiamali yake kwa jinai hiyo ya utawala haramu wa Israel, Harakkati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imesisitiza kkuwa, jinai hizo za Israel hazitakoma isipokuwa kwa kudumishwa muqawama na mapambano dhidi ya utawala huo dhalimu.

Madhumuni ya hujuma na uvamizi huo unaoendelea kila uchao ni kuandaa mazingira ya kutekeleza mpango mwovu wa kuugawanya msikiti mtukufu wa Al-Aqsa kimahali na kiwakati katika matumizi baina ya Waislamu na Mayahudi, ili hatimaye Wazayuni waweze kuudhibiti kikamilifu msikiti huo na kuchukua hatua zinazolenga kuuyahudisha na kuubomoa na kujenga kwenye magofu yake hekalu la uzushi la Kiyahudi.

4130797

Habari zinazohusiana
captcha