IQNA

Hadi al-Amiri

Wazayuni ndio chimbuko la njama dhidi ya taifa la Iraq

18:07 - April 30, 2022
Habari ID: 3475189
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Muungano wa Fat'h nchini Iraq amesema kuwa, kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel ni hatua ambayo haikubali kwa namna yoyote ile.

Hadi al-Amiri ameeleza kuwa, kwa mujibu wa matakwa ya wananchi wa Iraq, kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel ni jambo lisilokubalika.

Mkuu wa Muungano wa Fat'h nchini Iraq amesisitiza kuwa, Wazayuni ndio chimbuko la njama dhidi ya taifa la Iraq.

Hayo yanajiri siku chache tu baada ya mrengo wa Sadr unaoongozwa na mwanachuoni mashuhuri wa Kishia nchini Iraq, Muqtada al-Sadr kuandaa muswada wa sheria inayoharamisha kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

Muqtada al-Sadr ameeleza bayana kuwa, "Suala la kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel, na ndoto za utawala huo haramu kutaka kulitawala taifa letu pendwa la Iraq, ni moja ya sababu kuu za Harakati ya Sadr kujitosa kwenye mchakato wa uchaguzi."

Ikumbukwe kuwa, nchi nne za Kiarabu za Imarati (UAE), Bahrain, Morocco na Sudan mwaka 2020 zilisaini hati za makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni, hatua ambayo imeendelea kupingwa na kulaaniwa vikali katika nchi za Kiarabu na Kiislamu.

Sudan, Morocco na Bahrain zimeendelea kushuhudia maandamano kila leo ya wananchi ya kulaani na kupinga hatua ya nchi zao ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa  Israel. Wananchi waliowengi katika nchi hizo wanasema kuwa, hatua hiyo ni khiyana na usaliti mkubwa kwa wananchi wa Palestina wanaofanyiwa unyama wa kila aina na utawala wa Israel kila uchao.

4053760

captcha