IQNA

Pepo Katika Qur'ani /8

Chimbuko la Chemchemi za Peponi

22:26 - February 10, 2024
Habari ID: 3478331
IQNA - Kwa mujibu wa Surah Al-Insan ya Qur'ani Tukufu, waja wema wa Mwenyezi Mungu wanaweza kufanya chemchemi za peponi kutiririka kutoka popote wanapotaka.

Elimu ya kimungu na Marifat (elimu ya ukweli wa kiroho) ambayo huzipa uhai nyoyo za waumini, hudhihirika katika umbo la mito ya Peponi (Aya ya 15 ya Surah Muhammad).

Swali ni je, Qur’ani Tukufu inabainisha wapi mito hii inatoka?

Tunasoma katika Surah Hud, inapozungumzia kuumbwa kwa mbingu na ardhi, kwamba "Na Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Na Kiti chake cha Enzi (Arshi) kilikuwa juu ya maji." (Aya ya 7).

Ni wazi kuwa, Kiti cha Enzi cha Mwenyezi Mungu ambacho ambacho kiko katika Malakut si cha kiaumbile kama kiti cha kawaida cha kidunia ­­­­tunachokifahamu.­­ Kwa hivyo asili ya mito ya peponi inapaswa kuwa katika Arshi ya Mwenyezi Mungu na hili limebainishwa katika baadhi ya Hadithi pia.

Tunasoma katika Aya ya 6 ya Surah Al-Insan: “Ni chemchem watakao inywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakiifanya imiminike kwa wingi."

Inaweza kusemwa kwamba maji haya ni kutoka kwa kiti cha enzi cha kimungu na watumishi maalum wa Mungu wanaweza kufanya mito hii kutiririka.

Sasa swali ni je hawa watu maalum ni akina nani? Kinachofuata katika Surah Al-Insan, kinatupa dalili Fulani ya tukio la kihistoria: "Na wanawapa chakula masikini na mayatima na mateka kwa kumpenda." (Aya ya 8)

Wafasiri wengi wa Qur'ani kutoka katika madhehebu yote ya Kiislamu wamesimulia kwamba wakati mmoja Imam Hassan (AS) na Imam Hussein (AS) waliugua na walipopona watu wakamwambia baba wa wavulana hawa wawili, Imam Ali (AS) aweke Nadhiri .

 Imam Ali (AS) na Bibi Zahra (SA) waliweka Nadhiri ya kufunga siku tatu. Walifanya hivyo wakati Hassan  (AS) na Hussein (AS) walipopona. Wawili hao pia walifunga. Siku ya kwanza ilipofika wakati wa kufuturu, maskini mmoja alibisha hodi mlangoni mwao na kuomba chakula. Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (SAW) yaani Ahul Bayt walitoa walichokuwa nacho kwa masikini. Siku ya pili na ya tatu alikuja yatima na mateka na kuomba kitu cha kula, hapo pia wakawapa walichokuwa nacho na kulala njaa kwa siku tatu.

Siku ya nne, Mtukufu Mtume (SAW) aliwaona na akahuzunika. Wakati huo, Jibril  alikuja na akateremsha sura hii (Sura Al-Insan).

Hadithi hii imepokewa katika vitabu vya Shia na Sunni na Maswahaba na Tabi'un (kizazi cha Waislamu waliofuata maswahaba).

3487103

Kishikizo: qiyama
captcha